Wafuasi wa serikali wavamia bunge na kuwapiga wabunge Venezuela

Huwezi kusikiliza tena
Wabunge waliojeruhiwa venezuela

Karibu wafuasi 100 wa serikali wamevamia bunge linalodhibitiwa na upinzani nchini Venezuela ambapo waliwapiga wabunge.

Walioshuhudia walisema kuwa makabiliano hayo yalitokea baada ya kikao cha bunge kuadhimisha siku ya uhuru.

Polisi waliakuwa wakilinda bunge walitizama wakati wavamizi waliokuwa na fimbo walipovunja lango.

Serikali imeapa kufanya uchunguzi.

Karubi watu 350 walifungiwa ndani ya bunge kwa saa kadhaa wakiwemo waandishi wa habari, wanafunzi na wageni kwa mujibu wa spika wa bunge Julio Borges.

Bwana Borges aliwataka wabunge watano waliojeruhuwa. Baadhi walipelekwa kufanyiwa matibabu.

Venezuela imetikizwa na maandamano yenye ghasia miezi ya hivi karibuni na sasa inakumbwa na matatizo ya kuichumi.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Walioshuhudia walisema kuwa makabiliano hayo yalitokea baada ya kikao cha bunge kuadhimisha siku ya uhuru.

Wizara ya mashauri ya nchi za kigeni ililaani ghasia hizo ikizitaja kuwa dhuluma dhidi ya demokrasia inayofurahiwa na watu wa Venezuela tangu ipate uhuru miaka 206 iliyopita

Kabla ya wavamizi kuingia majengo ya bunge makamu wa rais Tareck El Aissami alionekana bungeni akiandamana na mkuu wa majeshi Vladimir Padrino Lopez.

Bwana El Aissami kisha akatoa hotuba akiwashauri wafuasi wa rais kuenda bungbni kumuonyesha raisu ungwaji mkono

Umati ulikuwa ukiandamana nje ya majengo ya bunge kwa saa kadhaa kabla ya kuingia ndani.

Mada zinazohusiana