ICC: Afrika Kusini ilistahili kumkamata Bashir

Rais Bashir Haki miliki ya picha AFP
Image caption Rais Bashir

Mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC imeamua kuwa Afrika Kusini, ilifanya makosa kwa kutomkamata rais wa Sudan Omar al-Bashir wakati alifanya ziara nchini humo mwaka 2015

Ilisema kuwa Bashir hakuwa na kinga ya kidiplomasia na hivyo angekamywa na kukabidhiwa kwa mkuu wa mashtaka kwa wa ICC kufuatia madai ya kuhusika kwenye mzozo wa jimbo la Darfur.

Serikali ya Rais Jacob Zuma, imesema kuwa masharti ya ICC yanaenda kinyume na sheria za nchi na kuwa imeanzisha mchakato wa kuondoka kutoka uanachama wa ICC, hatua ambayo makundi ya haki yanapinga.

Mahakama ya juu pia imeamua kuwa serikali imeenda kinyume na katiba kujiondoa kutoka ICC baada ya kushindwa kuomba ushauri wa bunge.

Jana chama tawala cha ANC, kilisema kuwa kina mpango ya kuiondoa nchi hiyo kutoka mahaka ya ICC.

Hii ni sehemu ya kampeni kubwa kutoka kwa baadhi ya nchi za kiafrika zinazodai kuwa ICC inawalenga viongozi wa bara la Afrika.

Mada zinazohusiana