Watu 8 wauwawa kwenye mkanyagano uwanja wa mpira Malawi

Watu 8 wauwawa kwenye mkanyagano uwanja wa mpira Malawi
Image caption Watu 8 wauwawa kwenye mkanyagano uwanja wa mpira Malawi

Watu wanane wakiwema watoto saba wameuwawa kwenye mkanyagano kabla ya kufanyika kwa mechi ya kandanda nchini Malawi.

Watu wengine zaidi walijeruhiwa wakati wa mkanyagano huo ulitokea uwaja wa Bingu mjini Lilongwe.

Mkanyagano huo unaripotiwa kutokea wakati maefu ya watu walijaribu kutafuta viti kabla ya mchuano wa kirafiki kati vilabu vikubwa vya Nyasa Big Bulets na Silver Strikers.

Rais Peter Mutharika ametuma rambi rambi zake na kusema kuwa serikali inafanya kila iwezalo kuzisadia familia za waliouawa.

Mwandishi wa BBC aliye Malawi anasema kwa milango ya uwanja huo unaowachukua watu 40,000 ilistahili kufunguliwa kuruhusu watu kuingia mapema lakini ilichelewa kwa muda wa saa tatu.

Hata hivyo maelfu walikwa wamefika na baadhi walijaribu kuingia kwa nguvu hali iliyosababisha polisi kufyatua vitoa machozi.

Inspekta wa polisi aliliambia shirika la Reuters kuwa anatarajia idadi wa waliokufa kuongezeka.

Image caption Watu 8 wauwawa kwenye mkanyagano uwanja wa mpira Malawi

Mada zinazohusiana