Tupac alidai Madonna alivunja uhusiano wao kwa sababu ya ubaguzi

Madonna na Tupac Shakur Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Madonna na Tupac Shakur

Tupac Shakur alimwambia msanii Madonna kwamba alivunja uhusiano wao wa kimapenzi kutokana na rangi ya ngozi yake katika barua iliojawa na hisia kwa msanii huyo wa muziki wa rap.

Barua hiyo ya 1995 ilioandikwa kwa ''M'' ilisema kuwa na mwanamume mweusi kungeweza kumsaidia kikazi lakini hatua hiyo itawaudhi mashabiki wake.

Madonna alithibitisha miaka miwili iliopita kwamba alikuwa na uhusiano na Tupac Shakur ijapokuwa haijulikani ulichukua muda gani.

Barua hiyo inapigwa mnada huku bei yake ya kwanza ikiwa $ 100,000.

Ikiwa imeandikwa tarehe 15 mwezi Januari 1995, iliandikwa wakati Tupac alipokuwa akihudumia kifungo jela kwa unyanyasaji wa kingono na ilijiri miezi 18 kabla ya yeye kuuawa kwa kupigwa risasi.

Haki miliki ya picha MOD
Image caption Msanii huyo aliuza rekodi milioni 75 duniani

Wasanii wote wawili walikuwa na umaarufu mkubwa na ''Kwa wewe kuonekana na mtu mweusi hakungedhuru kazi yako kivyovyote na badala yake kungefanya uonekana mtu uliye wazi na wa kufurahisha, Tupac aliyekuwa na umri wa miaka 23 alimwandikia Madonna akiwa katika Jela ya New York Clinton.

''Lakini kwangu mimi nilihisi kana kwamba kulingana na vile watu wanavyonichukulia ningewaudhi nusu ya watu walionifanya kuwa nilivyo',aliandika Madonna

''Kama ulivyosema, sijakuwa rafiki ambaye najua naweza kuwa'', aliandika Tupac , akiongezea, ''sikupenda kukuumiza moyo''.

Jarida la Rolling Stone lilithibitisha uhasilia wa barua hiyo ambayo ilichapishwa kwa mara ya kwanza na mtandao wa TMZ.

Tupac ambaye wazazi wake wote walikuwa wanaharakati wa Black Panther pia alisema kwamba Madonna wakati huo akiwa na umri wa miaka 36 alimuumiza moyo wakati aliposema katika mahojiano kwamba ''alikuwa amekwenda kuwabadili tabia wachezaji wote wa mpira wa kikapu pamoja na wasanii wote wa muziki wa rap''.

''Maneno hayo yaliniumiza moyo kwa sababu singedhani kwamba ulikuwa na uhisano mwengine na msanii yeyote wa rap isipokuwa mimi'', aliandika Tupac.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Tupac alifariki katika mfyatuliano wa risasi akiwa ndani ya gari

''Ni wakati huu ambapo baada ya kuumizwa moyo niliamua kujitetea na ndiposa nikasema mambo mengi''.

Aliongezea: tafadhali nielewe msimamo wangu wa awali kama kijana mdogo asiye na uzoefu.

Tupac alimalizia: Inafurahisha lakini uzoefu wangu umenifunza kutochukulia vitu vilivyo.

Mnamo mwezi Septemba tarehe 7 1996, msanii huyo ambaye aliuza rakodi milioni 75 duniani alifariki katika mfyatuliano wa risasi akiwa katika gari katika mji wa Las Vegas muda mfupi baada ya kutazama ndondi ambapo Mike Tyson alikuwa akizipiga.

Barua hiyo itapigwa mnada katika eneo la Gotta Have Rock and Roll Sale, ambao unatarajiwa kufanywa kati ya tarehe 18 na 19 mnamo mwezi Julai.