Wasiwasi kuhusu maduka ya jumla ya Nakumatt

Wasiwasi kuhusu maduka ya jumla ya Nakumatt

Nchini Kenya, maduka makubwa zaidi ya jumla katika ukanda wa Afrika Mashariki, Nakumatt, yanakumbwa na misukosuko ya kifedha inayohatarisha mustakabali wake.

Kwa sasa maduka hayo yanajitahidi kutafuta jinsi ya kulipa madeni ya zaidi ya dola millioni 170.

Kampuni inayomiliki maduka hayo imesimamisha mchakato wa kuajiri wafanyakazi wapya wakati ambapo ina wafanyakazi zaidi ya 5000, huku ikitafuta jinsi ya kujinasua kutoka kwa minyororo ya upungufu wa fedha.

Mwandishi wetu David Wafula ametuandalia ripoti ifuatayo.