Chupa za maji kuwa matofali
Huwezi kusikiliza tena

Njia mbadala ya kutumia chupa za plastiki za maji kujengea nyumba

Ni kawaida kwa nyumba kujengwa kwa kutumia matofali au katika baadhi ya maeneo ya vijijini kutumia udongo. Hata hivyo, katika hali isiyo ya kawaida, huko kaskazini mwa Tanzania, kikundi cha wanawake wanaojiita Kazi na Bobo wamebuni njia mbadala nayo ni yakutumia chupa za plastiki za maji kwa kujengea nyumba.

Kina mama hao ambao wanatoka kijiji cha Msitu wa Tembo, mkoani Manyara wanadai ujenzi huo unapunguza gharama na vile vile kuwaongezea kipato.

Mwandishi wa BBC,Esther Namuhisa hivi karibuni alikutana na kina mama hao na kutuandalia taarifa ifuatayo