Kifo cha Nkaissery: Matiang'i ateuliwa kaimu waziri wa usalama Kenya

Matokeo hayo yameonyesha kupungua kwa alama bora ikilinganishwa na miaka ya awali. Ni asilimia 15 tu ya wanafuzi wamefuzu kujiunga na elimu ya chuo kikuu kwa moja.
Image caption Waziri wa elimu nchini Kenya Fred Matiang'i

Waziri wa elimu nchini Kenya Dkt Fred Matiang'i ameteuliwa kuwa kaimu waziri wa usalama wa ndani kufuatia kifo cha aliyekuwa waziri Meja Jenerali Mstaafu Joseph Nkaissery.

Waziri huyo wa usalama alifariki dunia muda mfupi baada ya kulazwa katika hospitali ya kibinafsi ya Karen jijini Nairobi kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu.

Uteuzi wa Dkt Matiang'i umetangazwa na Rais Uhuru Kenyatta baada ya kuongoza mkutano wa dharura wa Baraza la Usalama wa Taifa.

Rais Kenyatta amesema hakutakuwa na pengo lolote kiusalama nchini kutokana na kifo cha jenerali huyo mstaafu.

Rais amesema maandalizi ya uchaguzi mkuu ambao utafanyika tarehe 8 Agosti, mwezi mmoja kuanzia sasa, yataendelea bila kuvurugika.

Bw Kenyatta amewataka Wakenya kuendelea kudumisha utulivu.

Mada zinazohusiana