Watu 9 wauwawa katika mpaka wa Somalia na Kenya

Ramani ya Kenya na Somalia
Image caption Ramani ya Kenya na Somalia

Kumekuwa na shambulio jengine kusini mwa Kenya karibu na mpaka wa Somalia, ambapo takriban watu tisa wameuawa.

Baadhi ya ripoti zinasema waliouawa wote ni raia, kwa risasi na baadhi kwa mapanga.

Eneo hilo katika kaunti ya Lamu limeshuhudia mashambulio kadhaa ambapo polisi wanaamini yamefanywa na kundi la al Shabaab kutoka Somalia.

Kundi hilo pia limelenga majeshi ya Kenya yenye vituo vyao hapo kama sehemu ya jeshi la Umoja wa Afrika.