G20: Viongozi watofautiana na Trump kuhusu makubaliano ya Paris

Viongozi waliokuwa katika mkutano wa G20 Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Viongozi waliokuwa katika mkutano wa G20

Viongozi wa mataifa 19 katika mkutano wa mataifa tajiri duniani G20 unaofanyika nchini Ujerumani wameweka upya ahadi yao ya kuidhinisha makubaliano ya Paris kuhusu mabadiliko ya tabia nchi , licha ya Marekani kujiondoa.

Tofauti miongoni mwa viongozi zilionekana katika siku ya miwsho mjini Hamburg lakini hatimaye makubaliano yaliafikiwa.

Mkutano huo ulitambua hatua ya Marekani ya kujiondoa katika makubaliano ya Paris bila kukandamiza juhudi za mataifa mengine.

Makubaliano hayo yaliafikiwa baada ya maandamano ya ghasia katika mji ulioandaa mkutano huo.

Makubaliano hayo ya pamoja yaliotolewa siku ya Jumamosi yalisema: Tunatambua hatua ya Marekani kujiondoa kutoka kwa makubaliano ya Paris.

Hatahivyo ,viongozi wa mataifa mengine ya G20 walikubaliana kwamba makubaliano hayo hayaweza kubadilishwa ili kuthibitisha mapatano hayo.

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel alisema kuwa anaunga mkono uamuzi wa rais Trump kuhusu makubaliano hayo ya Paris lakini akaongezea kwamba anafurahishwa kwamba viongoze 19 walipinga mpango huo kujadiliwa upya.

Alitaja mazungumzo ya kwanza siku ya Ijumaa kama ''magumu''.

Viongozi pia walifanya mazungumzo mjini hamburg mapema.

Rais Trump alikutana na waziri mkuu wa Uingereza Theresa May na kusema kuwa makubaliano ya kibiashara kati ya Marekani na Uingereza yatatiwa saini hivi karibuni.

Bwana Trump baada ya mkutano wake na Theresa May alisema kuwa anatarajia makubaliano yenye mkubwa wa kibiashara kati ya mataifa hayo mawili haraka iwezekanavyo.

Mkutano wa G20 unashirikisha mataifa 19 yalioendelea na yanayoendelea ikiwemo yale ya bara Ulaya.