Rais Putin: Nimeimarisha uhusiano wangu na Trump

Rais wa Urusi Vladmir Putin amesema kuwa ameimarisha ushirikiano wake na rais wa Marekani Donald Trump baada ya viongozi hao kuonana ana kwa ana G20
Image caption Rais wa Urusi Vladmir Putin amesema kuwa ameimarisha ushirikiano wake na rais wa Marekani Donald Trump baada ya viongozi hao kuonana ana kwa ana G20

Rais wa Urusi Vladmir Putin amesema kuwa ameimarisha ushirikiano wake wa kikazi na rais wa Marekani Donald Trump.

Bwana Putin alisema kuwa kufuatia mkutano wake na Donald Trump ana kila sababu ya wawili hao kuweka kiwango cha ushirikiano kinachohitajika.

Kiongozi huyo wa Urusi alisema kuwa usitishwaji wa mapigano kusini wa Syria uliotangazwa hapo jana unatokana na kile alichokitaja kuwa msimamo wa ushirikiano mzuri na Marekani .

Alisema kuwa rais huyo wa Marekani yuko tofauti sana katika maisha ya kawaida na alivyo katika runinga .

Pia amesema kuwa anaamini kwamba rais Trump amekubali hakikisho lake kwamba Moscow haikuingilia uchaguzi wa Marekani mwaka uliopita.