Kiongozi wa upinzani Leopoldo Lopez aachiliwa Venezuela

Venezuela's opposition leader Leopoldo Lopez salutes supporters outside his home in Caracas (07 July 2017) Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Bwana Lopez (juu) akishagiliwa na wafuasi wake mjini Caracas

Rais wa Venezuela Nicolás Maduro amepongeza hatua ya kumuachilia kutoka gerezani moja wa viongozi wakuu wa upanzani nchini humo Leopoldo Lopez.

Bwana Lopez amepelekwa katika kifungo cha nyumbani baada ya kukaa gereza kwa zaidi ya miaka mitatu.

Aliondoka gerezani karibu na mji wa Caracas na kujiunga na familia yake siku ya Jumamosi.

Bwana Lopez alikuwa akitumikia kifungo cha miaka 14 kwa kuchochea ghasia wakati wa maandamano ya kuipinga serikali mwaka 2014, mashtaka ambayo ameyakanusha. Mahakama kuu inasema kuwa ameachiliwa kwa misingi ya kiafya.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Lopez akiwa na watoto wake

Bwana Maduro alisema kuwa anaunga mkono na kuheshimu uamuzi wa mahakama lakini lakini akataka kuwepo kwa amani.

Saa chacahe baada ya kuichiliwa Bwana Lopez aliwashauri wafuasia wake kuendelea kuandamana barabarani kumpinga Bwana Maduro.

Akielezea maisha ya mwawawe gerezani babake Lopez aliiambia radio moja ya Uhispania siku chache zilizopita kuwa aliadhibiwa kwa kufungiwa katika chumba kisicho na mwangaza na maji kwa muda wa siku tatu.

Alisema kuwa mwamawe sasa alikuwa amefungiwa kifaa cha eletroniki ili mamlaka ziwezi kufuatilia mienendo yake.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Lopez alipigwa picha akishika bendera ya Venezuela

Mada zinazohusiana