Waziri mkuu wa Iraq Haider al-Abad awasili mji uliokombolewa wa Mosul

Waziri mkuu wa Iraq Haider al-Abad akiwasili mji uliokombolewa wa Mosul Haki miliki ya picha IRAQ PM OFFICE/TWITTER
Image caption Waziri mkuu wa Iraq Haider al-Abad akiwasili mji uliokombolewa wa Mosul

Waziri mkuu nchini Iraq Haider al-Abadi amewasili mjini Mosul kuwapongeza wanajeshi wa Iraq kwa ushindi wao dhidi a kundi Islamic State nchini humo.

Bwana Abadi alikuwa mjini humo kutangaza ukombozi na ushindi, kwa mujibu wa ofisi ya rais.

Vikosi vya Iraq vinavyoungwa mkono na mashambulizi ya Marekani vimekuwa vikipigana kuukomboa mji wa Mosul tangu tarehe 17 mwezi Oktoba mwaka uliopita

Mwaandishi wa habari wa BBC anasema kuwa, milio ya risasi inasikika katika baadhi ya mitaa ya mji huo huku, ushindi mkuu na wa mwisho wa kukamilisha ukombozi wa mji huo unatazamiwa kutangazwa na utawala wa nchi hiyo wakati wowote sasa.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Polise wameamza kusherehekea mitaani

Kamanda mmoja mkuu wa jeshi la Iraq, amesema kuwa wanajeshi wa Iraq kwa ujumla, wamekamilisha operesheni hiyo katika mji wa kale wa Mosul, ambao ulikuwa eneo la mwisho kwa I-S kuushikilia.

Wanajeshi wameonekana wakipepeza angani bunduki zao, huku wakisherehekea ushindi, katika barabara za mji huo, ambao majengo mengi yameporomoshwa na mizinga.

Raia wameonekana pia wakitembea, baada ya kutoka katika vifusi vya majengo hayo.

Lakini kumesikika milio ya risasi, katika baadhi ya maeneo, huku tangazo rasmi la mwisho la seriali ya kukamilisha mapigano hayo, bado halijatolewa.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Polisi mjini Mosul

Mada zinazohusiana