Madaktari watofautiana kuhusu matibabu ya Liu Xiaobo

A woman holds a candle as she attends a vigil for terminally-ill Nobel laureate Liu Xiaobo (pictured on banner) in Hong Kong on June 29, 2017 Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Wafuasi wameomba China kumruhusu Bwana Liu kuenda kupata matibabu

Madaktari wawili kutoka nchi za magharibi wametofautiana na madaktari wa kichina kuhusu hatma ya mshindi wa tuzo la amani la Nobel mgonjwa wa saratani ya ini.

Liu Xiaobo, ambaye ni mfungwa aliyekuwa akitetea democrasia alipelekwa hospistalini akiwa anatumikia kifungo cha miaka 11, kutokana na ugonja ambao umefikia hali mbaya wa saratani ya ini.

Madaktari wake nchini China wanasema kuwa yeye ni mgonjwa sana kuweza kusafirishwa ng'ambo na ni lazima abaki nchini China.

Lakini madaktari kutoka Marekani na Ujerumani ambao walimfanyia uchunguzi bwana Liu wanapinga wakisema kuwa anaweza kusafirishwa.

Haki miliki ya picha Posted on Twitter by Guangzhou-based writer Ye Du
Image caption Liu Xiaobo na mkewe

Madaktari hao wanasema kuwa bwana Liu anaweza kusafirishwa lakini kwa haraka sana.

Liu Xiaobo na familia yake wote wameamba aruhusiwe kusafiri.

Bwana Liu alikuwa kiongozi mkuu kwenye maandamano ya Tiananmen mwaka 1889 na tangu wakati huo amekuwa akipigania kuwepo kwa demokrasia kamili nchini China.

Serikali inamtambua kuwa mhalifu na mwaka 2009 ilimhukumu kifungo cha miaka 11 jela.

Haki miliki ya picha Supplied
Image caption Liu Xiaobo na mkewe Liu Xia

Mada zinazohusiana