Maelfu waandamana dhidi ya Rais Erdogan Uturuki

Erdogan amekuwa Rais wa Uturuki tangu mwaka 2014
Image caption Erdogan amekuwa Rais wa Uturuki tangu mwaka 2014

Maelfu ya watu wameandama katika mji wa Istanbul nchini Uturuki dhidi ya Rais wa nchi hiyo Recip Tayyip Erdogan.

Akihutubia katika maandamano hayo, kiongozi mkuu wa upinzani Kemal Kilicdaroglu, ameishutumu serikali kwa mfululizo wa kukamatwa na kufungwa kwa watu ikiwa ni matokeo ya jaribio la mapinduzi lililoshindikana mwaka jana.

Image caption Maelfu pia waliandamana kumpinga Erdogan alipotembelea Marekani hivi karibuni

Amesema raia wa Uturuki wanaishi chini ya Udikteta.

Rais Erdogan maandamano hayo yanaunga mkono ugaidi.