Marufuku ya laptopu yaondolewa mashirika 2 ya ndege yanayoelekea Marekani

Customers walk past Kuwait Airways board in Kuwait Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Marufuku ya laptopu yaondolewa mashirika 2 yanayoelekea Marekani

Mashirika ya Kuwait Airways na Royal Jordanian yamekuwa ya hivi punde kuruhusu abiria kubebea laptopu ndani ya ndee zinazoelekea Marekani.

Mashirika hayo mawili yalisema yameshirikiana na maafisa wa Marekani kuimarisha usalama kwa ndege zinazotoka nchini Kuwait na Jordan.

Marekani ilitangaza marufuku hiyo mwezi Machi kwa safari za moja kwa moja kutoka nchi nane za kiislamu kutokana na hofu kuwa mabomu yangebebwa ndani ya vifaa hivyo.

Mashirika ya ndege ya Etihad, Turkish Airlines, Emirates and Qatar yaliondolewa marufuku hiyo wiki iliyopita.

Shirika la Royal Jordanian ambalo hufanya safari katika miji mitatu ya Marekani kutoka Amman, mji mkuu wa Jordan, liliondoa marufuku hiyo baada ya hatua mpya za kiusalama zilizochukuliwa kwenye ndege zinazoelekea nchini Marekjni.

Shirika linalomikiw na serikali la Kuwait Airlines ambalo hufanya safari zake kutoka Kuwait kuenda mjini New York likipitia Ireland lilisema kuwa marufuku hiyo ilitolewa baada ya maafisa wa Mareknian kukagua usalama kwenye safari zake.

Mada zinazohusiana