Video ya kwanza ya wanawake watumwa wa ngono wa Korea yatolewa

China Haki miliki ya picha US National Archives

Korea Kusini imetoa kile inachokitaja kuwa kanda yake ya kwanza ya wanawake waliolazimishwa kuwa watumwa wa ngono na wanajeshi wa Japan wakati wa vita vya pili va dunia.

Kanda hiyo iliyorekodiwa na wanajeshi wa Marekani nchini China, ilipatwa na wachunguzi waliofadhiliwa na serikali katika chuo cha Seoul kwenye kumbukumbu za Marekani.

Kanda hiyo ya sekunde 18 inaonyesha wanawake kadha wakiwa wamejipanga wakizungumza na mwanajeshi wa China.

Wanaharakati nchini Korea Kusini wanakadiria kuwa wanawake 200,000 walilazimishwa kufanya kazi katika madanguro ya wanajeshi wa Japan.

Wanaaminika kutokea nchini Korea, lakini pia kutoka nchini China, Indonesia , Ufolipino na Taiwan.

Hadi sasa kumbukumbu za wanawake waliolazimishwa kuwa watumwa wa ngono na wanajeshi wa Japan wakti wa vita vya pili vya dunia imekuwani picha na ushuhuda.

Haki miliki ya picha US National Archives
Image caption Video ya kwanza ya wanawake watumwa wa ngono yatolewa

Mada zinazohusiana