Tatizo la intaneti lailetea Somalia hasara kubwa

Tatatizo la intaneti lailetea Somalia hasara kubwa
Image caption Tatatizo la intaneti lailetea Somalia hasara kubwa

Waziri wa mawasiliano nchini Somalia ametangaza kuwa tatizo la kupotea kwa intaneti, kwa muda wa karibu wiki mbili sasa ni janga kubwa kwa uchumi wa nchi hiyo.

Abdi Anshur Hassan, aliiambia radio ya taifa kuwa nchi inapoteza takriban dola milioni 10 kwa siku kutokana na kukatika kwa internet na hadi sasa nchi imepoteza dola milioni 130.

Tatizo hilo lilisababishwa na kuharibiwa kwa nyaya za chini ya bahari zaidi ya wiki mbili zilizopita, kwa mujibu wa Radio Mogadishu.

Hata hivyo Bwana Hassan anasema kuwa serikali inafanya kila iwezalo kurejesha huduma hiyo.

Mada zinazohusiana