Wasichana waonywa dhidi ya kupotoshwa na mitandao ya kijamii Nigeria

Sultan wa Sokot Alhaji Saad Abubakar Haki miliki ya picha AFP
Image caption Sultan wa Sokot Alhaji Saad Abubakar

Kiongozi wa dini wa cheo cha juu nchini Nigeria, Sultan wa Sokoto, amewaonya watoto, hususan wasichana wasije wakatumia muda wao mwingi kwenye mitandao ya kijamii kwa kuwa inaweza kusababisha upotovu wa maadili.

Akiongea wakati wa mashindano ya kusoma Koran katika mji wa Sokoto, Alhaji Saad Abubakar alisema kuwa ni jambo la kutia wasi wasi wakati mitandao ya kijamii kama Facebook, WhatsApp, Instagram na 2Go, inawapoteza wanafunzi kutoka kwa masomo yao.

"Wasichana ndio nguzo ya jamii na kama watapotoshwa, hiyo itakiwa hatari kubwa kwa jamii," alisema Alhaji Saad Abubakar.

Amewashauri wazazi kuhakikisha kuwa mabinti wao wanatumia muda mwingi kufanya vitu vya kuwafaidi, ikiwemo kusoma Koran kwa sababu hiyo itawafanya kuwa wazazi na watunzi wema.