Mbunge aliyedaiwa kumtusi Magufuli apewa dhamana Tanzania

Halima Haki miliki ya picha HALIMA MDEE/FACEBOOK

Mbunge wa chama cha upinzani nchini Tanzania cha Chadema Halima Mdee ameachiwa kwa dhamana katika mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam.

Aliachiliwa huru kwa dhamana ya shilingi milioni kumi za Tanzania na kesi dhidi ya yake ikaahirishwa hadi Agosti 7, 2017.

Awali mbunge huyo wa Kawe alisomewa shitaka la kutimia lugha ya matusi dhidi ya Rais John Magufuli.

Mbunge huyo wa upinzani alikamatwa na kushikiliwa wiki iliyopita kwa amri ya Mkuu wa wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam Ally Hapi ambaye alimshutumu Mdee kwa kumtolea lugha ya matusi Rais Magufuli.

Bi Mdee anadaiwa kutoa kauli za uchochezi alipokuwa akiongoza kikao cha Baraza la Wanawake Chadema jijini Dar es Salaam.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii