UN yaitaka Marekani kuondoa vikwazo Sudan

Omar al Bashir amekuwa madarakani toka mwaka 1993
Image caption Omar al Bashir amekuwa madarakani toka mwaka 1993

Wawakilishi wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan wamesema kuwa wanatumai Marekani itaondoa vikwazo dhidi ya taifa hilo.

Rais Trump ataamua siku ya Jumatano iwapo aongeze ama aondoe kabisa vikwazo vilivyowekwa na mtangulizi wake Obama.

Wawakilishi hao wamesema kuwa Sudan imeweza kutoa ulinzi na ushirikiano wa kutosha katika maeneo ambayo hayakufikika awali kutokana na vita.

Baadhi ya wanaharakati wanasema kuwa kuiwekea vikwazo Sudan ni kuwaongezea matatizo wananchi wake na sio Rais wa nchi hiyo anayetakiwa na mahakama ya uhalifu wa kimataifa Omar al Bashir.