Haider al-Abadi: Mosul bado ina changamoto nyingi

Haider al-Abadi alitembelea mji huo baada ya mapigano kumalizika
Image caption Haider al-Abadi alitembelea mji huo baada ya mapigano kumalizika

Waziri Mkuu wa Iraq, Haider al-Abadi, ametahadharisha kwamba kuna changamoto nyingi, licha ya ushindi katika mapambano ya kuurudisha mji wa Mosul kutoka katika himaya ya wapiganaji wa Kiislamu.

Mapigano ya miezi tisa yameharibu mji wa Mosul huku maelfu wakiwa wameukimbia mji huo na wengine wakiachwa bila makazi.

Akizungumza mjini humo, bwana Abadi amesema hivi sasa ni muhimu kurudisha hali ya utulivu.

Image caption Mapigano hayo yameuachia mji wa Mosul makovu makubwa

Kiongozi wa vikosi vinavyoongozwa na Marekani, jenerali Stephen Townsend, amesema vita dhidi ya wapiganaji wa kiislamu bado havijaisha.

Ameitaka serikali ya Iraq kuzungumza na waislamu wa dhehebu la Sunni ili kuepusha kuibuka tena kwa wapiganaji wa IS.