Trump anatarajiwa kufanya ziara Uingereza mwaka 2018

Donald and Melania Trump Haki miliki ya picha AFP
Image caption Trump anatarajiwa kufanya ziara Uingereza mwaka 2018

Rais wa Marekania Donald Trump anatarajiwa kufanya ziara nchini Uingereza mwaka ujao.

Bwana Trump alikubali mwaliko wa Malkia wa kumuomba afanye ziara nchini Uingereza wakati waziri mkuu Theresa May alifanya ziara nchini Marekani mwezi Januari.

Lakini ziara hiyo ilizua utata na hadi hata kusababisha Trump kubadili fikra zake.

Inaripotiwa kuwa hakutaka kuifanya ziara hiyo wakati kuna upinzani dhidi yake.

Mwezi Mei karibu watu milioni mbili walisaini ombi la kusema kuwa Trump haruhusiwa kuingia nchini Uingereza.

Wanasiasa wakuu akiwemo kiongozi wa chama cha Labour Jeremy Corbyn, na aliyekuwa kiongozi wa chama cha Lib Dem Tim Farron walitaka ziara hiyo kufutwa.

Maswali yaliibuka kuhusu ni kwa nini Trump alialikwa muda mfupi baada ya kuingia ofisini.