Bobi Wine kuapishwa kama mbunge Uganda

Wine aliwania kiti hicho kama mgombea huru na kuwashinda wagombea wanne ambapo alipata kura 25,659 kati ya kura 33,310 zilizopigwa Haki miliki ya picha Bobi Wine
Image caption Wine aliwania kiti hicho kama mgombea huru na kuwashinda wagombea wanne ambapo alipata kura 25,659 kati ya kura 33,310 zilizopigwa

Mwanamuziki wa nyimbo za reggae nchini Uganda Robert Kyagulanyi Ssentamu, maarufu kama Bobi Wine, anaapishwa leo kama mnunge wa eneo la Kyadondo East

Wine aliwania kiti hicho kama mgombea huru na kuwashinda wagombea wanne ambapo alipata kura 25,659 kati ya kura 33,310 zilizopigwa kwenye uchaguzi mdogo uliofanyika tarehe 29 mwezi Juni.

Alisema kuwa anaingia bungeni kama kiongozi na wala si mwanasiasa, kwa mujibu wa gazeti la New Vision.

Chama tawala NRM na upinzani wamekuwa wakimtaka Wine ajiunga na mmoja wao.

Picha ya Wine akimsalamia Rais Museveni wakati wa misa ya mfanyabiashara mmoja ilikosolewa na baadhi ya wafuasi wake katika mitandao.

Mada zinazohusiana