Urusi kuwatimua wanadiplomasia 30 wa Marekani

US President Donald Trump (R) speaks with Russian President Vladimir Putin at G20 in Hamburg, 7 Jul 17 Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mkutano wa kwanza kati ya Putin na Trump mjini Hamburg wiki iliyopita

Urusi iko tayari kuwatimua wanadiplomasia 30 wa Marekani na kutwa mali ya Marekani kujibu vikwazo vya Marekani, kwa mujibu wa maafisa wa Urusi.

Vitisho hivyo vinatolewa kutoka wizara ya mashauri ya nchi za kigeni ya Urusi na kunukuliwa na gazeti la daily Izvesta.

Mwezi Disemba utawala wa Obama uliwatimua wanadiplomasia 35 wa Urusi na kufunga makao mawili ya kijasusi.

Hatua hizo ni jibu kwa madai ya kuwa Urusi iliingilia uchaguzi wa Marekani.

Urusi tayarai iko chini ya vikwazo vya Marekani.

Timu ya Trumo hayo iko chini ya uchunguzi kufuatia madai ya Urusi kuingia kati kampeni ya mwaka uliopita. Hata hivyo Urusi imekana madai hayo.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Makao ya Urusi huko Maryland yalitwaliwa na serikali ya Marekani mwezi Disemba

Mada zinazohusiana