Ujumbe wa Ufaransa wanyimwa Visa na Rwanda

Bendera mpya ya Rwanda Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Bendera mpya ya Rwanda

Ujumbe wa kidiplomasia wa taifa la Ufaransa hivi majuzi ulipata pigo la kupata Visa baada ya mamlaka ya Rwanda kukataa ombi lao walilowasilisha ambalo lilishirikisha picha ya bendera ya zamani ya taifa hilo ambayo ilitumika wakati wa mauaji ya halakiki ya 1994 kulingana na ripoti za jarida la Jeune Afrique.

Gazeti hilo limeelezea hatua hiyo kama vuta ni kuvute ya kwanza katika uhusiano kati ya utawala huo mpya wa Ufaransa na Kigali.

Linasema kuwa mnamo terehe 9 na 10 ujumbe rasmi wa Ufaransa ulitarajiwa kusafiri kuelekea Cameroon kupitia Kigali .

Ujumbe huo ulishirikisha Mkurugenzi wa eneo la Afrika na bahari Hindi katika wizara ya maswala ya kigeni ,mkurugenzi wa eneo la jangwa la Sahara chini ya idara ya maendeleo nchini Ufaransa pamoja na mshauri wa kiuchumi ambao walitarajiwa kukutana na waziri wa mswala ya kigeni nchini Rwanda Luoise Mushikwabo mjini Kigali.

Mapema mwezi Julai, waziri wa maswala ya kigeni nchini Ufaransa aliwasilisha ombi la Visa kwa ubalozi wa Rwanda mjini Paris pamoja na ujumbe wao.

Katika kila taifa walilotembea kulikuwa na picha ya bendera.

Bendera ya Rwanda iliochapishwa ilikuwa kamili na rangi tatu za kijani, manjano na nyekundu ikiwa na herufi kubwa ya R katikati.

Image caption Bendera ya zamani ya Rwanda

Tatizo, hatahivyo ni kwamba Rwanda ilibadilisha bendera yake 2001.

Ile iliopo katika makavazi ya Ufaransa ni ile iliotumiwa na aliyekuwa rais wa taifa la Rwanda Juvenal Habyarimana.

Jeune Afrique linasema kuwa wakati walipowasiliana na wizara ya maswala ya kigeni hawakukana kwamba safari hiyo ilikuwa imeahirishwa.

Maelezo yao ni kwamba kutokana na makosa ya mamlaka Visa hizo hazikuweza kutolewa kwa muda unaofaa.kulingana na duru zilizokuwa na maelezo.

''Imeahirishwa na sio tatizo la kidiplomasia'', Afisa mmoja wa Rwanda ambaye hakutajwa na gazeti hilo alinukuliwa akisema.

Mada zinazohusiana