Mkewe rais Buhari awaonya ''maafisa wanaopigania kiti cha mumewe''Nigeria

Mkewe rais Buhari na mumewe
Image caption Mkewe rais Buhari na mumewe

Mke wa rais wa Nigeria amewaonya ''mafisi na mbwa mwitu'' kwamba watafukuzwa katika mtandao wa facebook akiwalenga maafisa wa serikali ya mumewe.

Matamshi ya Aisha Buhari yanadaiwa kulenga moja kwa moja maafisa wakuu wa chama tawala kulingana na mwandishi wa BBC Naziru Mikailu, katika mji mkuu wa Abuja.

Yanaonekana kuwa ya maafisa wanaopigania urais na naibu wake wakati ambapo mumewe ni mgonjwa.

Rais Muhammadu Buhari amekuwa mjini London akipokea matibabu.

Naibu wake amekuwa akichukua mahali pake wakati rais yuko nje lakini hakuna madai yoyote kutoka kwa Bi Buhari kwamba amekuwa akipanga njama dhidi ya mumewe kulingana na ripota huyo wa BBC.

Mada zinazohusiana