Mwana wa Trump alipewa ''habari'' za Clinton na Urusi

Mwana wa Donald Trump
Image caption Mwana wa Donald Trump

Mwana wa rais wa Marekani Donald Trump ametoa barua pepe inayoonyesha alipewa habari yenye siri kubwa kuhusu bi Hillary Clinton na raia mmoja wa Urusi.

Mchapishaji Rob Goldstone alimwambia Donald Trump Jr kwamba kuna habari ambayo ni miongoni mwa uungwaji mkono wa Urusi kwa rais Donald Trump.

Maafisa wa Marekani wanachunguza madai ya Urusi kuingilia uchaguzi wa Marekani.

Bwana Goldstone awali alikana kujua habari zozote ama kuhusishwa na serikali ya Urusi katika uchaguzi huo.

Barua pepe hiyo iliotumwa kwa bwana Trump Jr ambayo aliitoa katika mtandao wa twitter inasema kuwa kiongozi wa mashtaka nchini Urusi alikuwa amejitolea kuipatia kambi ya rais Trump nakala na habari ambazo zitamtia mashakani Hillary Clinton na uhusiano wake na Urusi na kwamba zitakuwa na usaidizi mkubwa kwa babake.

Bwana Trump alijibu: Iwapo hilo ndilo unalosema basi naipenda.

Urusi haina kiongozi mkuu wa mashtaka [Crown Prosecutor] lakini ina mkuu wa mashtaka {Prosecutor general}.

Mgombea wa chama cha Democrat bi Hillary Clinton alipoteza uchaguzi huo kwa rais Trump.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii