UN: Ukanda wa Gaza haukaliki kwa wakazi milioni mbili

Huduma muhimu za kibinaadamu hazipatikani kutokana na miundombinu kuharibiwa
Image caption Huduma muhimu za kibinaadamu hazipatikani kutokana na miundombinu kuharibiwa

Umoja wa Mataifa umesema Ukanda wa Gaza haukaliki kwa wakazi wake wapatao milioni mbili.

Katika ripoti inayoangalia hali ya kibinadamu, Umoja wa Mataifa umesema kiwango cha kipato, huduma ya afya, elimu, huduma ya umeme na maji safi ya kunywa imezorota katika kipindi cha miaka kumi tangu Hamas ichukue madaraka katika eneo hilo.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Maisha yamekuwa magumu kila kukicha

Baada ya kuchukua utawala, Israel ambayo inaitambua Hamas kama kundi la kigaidi, ikishirikiana na Misri wameitenga Gaza.

Mamlaka ya Palestina, ambayo inadhibiti eneo la West Bank imesitisha uhamishaji wa fedha katika ukanda huo wa pwani na kuitaka Israel kupunguza huduma ya umeme.