Maofisa Polisi wakamatwa kwa unyanyasaji Ureno

Maofisa hao wanatuhumiwa kwa ubaguzi wa rangi
Image caption Maofisa hao wanatuhumiwa kwa ubaguzi wa rangi

Timu nzima ya maofisa wa polisi nchini Ureno waliokuwa zamu katika kituo kimoja cha polisi wameshtakiwa kwa makosa ya kuwafungwa kimakosa, kuwadhihaki na kuwatesa watu watano weusi waliofika katika kituo hicho kwa malalamiko ya kuwekwa kizuizini kwa rafiki yao aliyetoka katika mji wa Shanty mji ulio karibu na mji mkuu Lisbon.

Waendesha mashtaka katika mji huo wanasema kwamba maofisa hao wapatao kumi na nane walitumia vibaya madaraka yao kwa kuwashikilia wanaume hao, ambao wanakadiriwa kuwa na umri wa miaka ishirini, kwa siku mbili mnamo mwezi February 2015 na baadaye Kusema uongo juu ya yale waliyowatendea .

Taarifa zinaeleza kuwa maofisa hao wanashutumiwa vikali kwa ubaguzi wa rangi.

Makazi hayo yasiyo rasmi, yaitwayo Cova de Moura, ni makaazi ya wahamiaji wengi kutoka Cape Verde, koloni la zamani la Ureno kutoka kaskazini Magharibi mwa Afrika.