Makamu Rais Yemi Osinbajo amtembelea Buhari London

Muhammadu Buhari na makamu Rais Yemi Osinbajo Abuja Machi 13,2017
Image caption Muhammadu Buhari na makamu Rais Yemi Osinbajo Abuja Machi 13,2017

Rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari ambae yuko London kwa ajili ya matibabu, amefanya mkutano wake wa kwanza na anaye kaimu nafasi hiyo kwa miezi miwili sasa.

Msemaji wa kaimu Rais, Yemi Osinbajo, ameelezea kuwa mkutano huo ulikuwa mzuri.

Hata hivyo, hakutoa maelezo zaidi.

Image caption Buhari alirejea kazini mwezi Machi baada ya matibabu London

Buhari amekuwa jijini London tangu mwezi Mei, akipata matibabu kwa ugonjwa ambao haujatajwa.

Bwana Osinbajo anategemewa kurudi nchini Nigeria baada ya mkutano huo.

Ukimya wake umeibua mjadala nchini Nigeria iwapo Buhari ataweza kurudi na kuendelea na majukumu yake ama la.

Image caption Buhari akiwa na familia yake mwezi Machi