Trump: Sikufahamu lolote kuhusu mkutano wa Junior

President Trump and son Donald Trump Junior embrace Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Trump: Sikufahamu lolote kuhusu mkutano wa JuniorTrump: Sikufahamu lolote kuhusu mkutano wa Junior

Mtoto wa kiume wa rais wa Marekani Donald Trump, amesema kuwa hakumfahamisha babake kuhusu mkutano na wakili raia wa Urusi ambaye alisema kuwa angesaidia katika kampeni yake ya uchaguzi

Donald Trump junior alikiambia kituoa cha habari cha Fox News kuwa mkutano huo haukuhusu chochote.

Alitoa barua pepe zake zikionyesha kuwa alikaribisha ombi la kukutana na wakili, ambaye alikuwa na uhusiano na Urusi, ambaye alikuwa na ujumbe potovu kumhusu Hillary Clinton.

Maafisa wa Marekani wanachunguza madai ya Urusi kuingilia uchaguzi wa Marekani.

Tangu achaguliwe Rais Trump ameandamwa na madai kuwa Urusi ilijaribu kuhujumu kampeni ya Bi Clinton.

Amekana kufahamu lolote na Urusi mara kwa mara imekana kungilia kampeni.

Alipoulizwa ikiwa alimuambia babake kuhusu mkutano wa mwaka uliopita, Bwana Trump junior alisema hakukuwa na chochote cha kumuambia.

Donald Trump Jr, mkwe wake Jared Kushner na mwenyekiti wa kampeni Paul Manafort, walikutana na wakili wa Urusi Natalia Veselnitskaya, katika jumba la Trump Tower mjini New York mwezi Juni mwaka 2016.