Jeshi la China laelekea kuweka kambi ya kwanza ya kigeni Djibouti

Picture of Chinese naval personnel in Djibouti in 2015 Haki miliki ya picha China News Service
Image caption Wanajeshi wanamaji wa China

Meli zinazowasafirisha wanajeshi wa China zinaelekea nchini Djibouti kuweka kambi ya jeshi ya China ambayo ndiyo ya kwanza ya kigeni.

China inasema kuwa kambi hiyo itatumiwa kwa huduma za kulida amani na za kibinadamu barani Afrika na magharibi mwa Asia.

Pia itatumiwa kwa ushikiano wa kijeshi, mazoezi ya kijeshi na huduma za uokoaji.

China imewekezaa katika nchi za kiafrika na pia imeboresha kwa haraka jeshi lake miaka ya hivi karibuni.

Image caption Djibouti

Shirika la habari ya Xinhua lilisema kuwa meli hizo ziliondoka bandari ya Zhanjiang katika mkoa wa kusini wa Guangdong siku ya Jumanne.

Halikutaja idadi ya wanajeshi au meli zilizoplelekwa Djibouti au ni lini kituo hicho kitaanza kutangaza huduma zake.

Xinhua linasema kuwa kituoa hicho cha Djibouti kinabuniwa kufuatia mazungumzo kati ya nchi hizo mbili.

Kituo hicho kinaonekana kama hatua ya China ya kuwa na usemi wa kijeshi eneo hilo.

Haki miliki ya picha AFP/Getty Images
Image caption China imejenga reli inayoungasha Djibouti na Addis Ababa

Mada zinazohusiana