Nusura ndege ya Canada igonge ndege nne uwanjani San Francisco

Air Canada planes. Archive photo Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Nusura ndege ya Canada igonge ndege nne uwanjani San Francisco

Idara inayohusika na safari za ndege nchini Marekania FAA ,inachungunza kisa ambapo ndege ya shirika la Air Canada nusura igonge ndege zingine katika uwanja wa San Franciso.

Shirika hilo linasema kuwa ndege ya AC759 ikitokea Toronto iliruhusiwa kutua siku ya Ijumaa lakini rubani akajianda kutua katika barabara ambapo ndege zingine zilikuwa zinajianda kupaa.

Waelekezi wa safari za ndege waliweza kufahamu tatizo hilo na kumuamrisha rubani kupaa tena ili kujiandaa kutua kwa kwa mara ya pili.

Kisha ndege hiyo ikaweza kutua salama.

FAA kwa sasa inachunguza umbali uliokuw kati ya ndege ya Air Canada na ndege iliyokuwa ikijiandaa kupaa.

Kisa hicho kinatajwa kuwa kisicho cha kawadia.

Air Canada inasema kuwa abiria 135 na wahudumu 5 walikuwa ndani ya ndege hiyo.

Haijulikani ni watu wangapi waliokuwa ndani ya ndege nne zilizokuwa kwenye barabara ya kupaa.

Image caption Nusura ndege ya Canada igonge ndege nne uwanjani San Francisco