Ngo'mbe wa maziwa wasafirishwa kwa ndege kwenda Qatar

Cows Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Ngo'mbe wa maziwa 165 wasafirishwa kwa ndege kuenda Qatar

Ng'ombe wamesafirishwa kwa njia ya ndege kwenda nchini Qatar kuongeza uzalishaji wa maziwa wakati taifa hilo linaendelea kutengwa na Saudi Arabia.

Ng'ombe 165 aina ya Holstein wamewasili kutoka nchini Ujerumani wakiwa ndio wa kwanza kati ya ng'ombe 4,000 wanaotarajiwa kusafirishwa kwenda Qatar.

Vizuizi vya angani, baharini na ardhini, vimesababisha wasi wasi nchini Qatar, nchi ambayo hutegemea kuagiza bidhaa kutoka nje kuweza kuwatimizia mahitaji wakaazi wake milioni 2.7.

Kundi la nchi zinazoongozwa na Saudi Arabia limeonya kuchukua hatua mpya dhidi ya Qatar baada ya kukataa masharti yake,.

Ng'ombe hao waliwasili kupitia ndege ya mizigo ya Qatar Airways siku ya Jumanne na kupelekwa makao maalum yaliyojengwa.

Kampuni ya Power International imenunua ng'ombe hao huku mwenyekiti wake Moutaz al-Khayyat akikiambia kituo cha Bloomberg kuwa wakati ng'ombe wote watakuwa wamewasili watachangia asilimia 30 ya mahitaji yote ya bidhaa za maziwa nchini humo itatimizwa.

Bidhaa hizo zitauzwa chini ya nembo mpya ambayo bwana al-Khayyat ameanzisha.

Mada zinazohusiana