Trump ashtakiwa kwa kuwazuia wakosoaji katika Twitter

A picture showing the masthead of President Donald Trump's @realDonaldTrump Twitter account Haki miliki ya picha @realDonaldTrump/Handout via REUTERS
Image caption Akaunti ya Trump ya Twitter ina wafuasi milioni 33.7

Rais wa Marekani Donald Trump kwa muda wa miaka 30 amekabiliwa na zaidi ya na kesi 4,000

Na sasa mwanabiashara huyo ambaye sasa ni Rais, ameshtakiwa kwa mara nyingine, baada ya watu saba kumshtaki kwa kuwazuia kwenye akaunti yake ya twitter.

Bwana Trump ni mtumiaji mkubwa wa mitandao ya kijami ambayo anaituma kuwapongeza washirika na kuwashambulia mahasimu wake.

Kesi hiyo iliwasilishwa mahakamani na taasi ya Knight First Amendment Institute, ambalo ni kundi la kupigania uhuru wa kusema katika chuo cha Columbia.

Watumiaji hao saba walisema kuwa akaunti zao zilifungwa na rais au wasaidizi wake, baada ya wao kukejeli au kukosoa ujumbe alioandika Trump.

Watumiaji wa Twitter hawan uwezo wa kuona au kujibu ujumbe katika akaunti zinazowazuia.

Mashtaka hayo ni kuwa kwa kuwazuia watu hawa, Bwana Trump amewazuia kujiunga na majadiliano ya mtandaoni.

Mada zinazohusiana