Kipande kikubwa cha barafu chameguka Antarctica

Larsen C crack Haki miliki ya picha NASA / SUOMI NPP / SIMON PROUD
Image caption Picha za barafu hiyo iliyopigwa na satelaiti ya Suomi NPP inayomilikiwa na NASA

Kipande kikubwa zaidi cha barafu kuwahi kuonekana duniani kimemefuka kutoka kwenye eneo la Antarctica.

Jiwe hilo kubwa la barafu linakadiriwa kuwa na ukubwa wa kilomita mraba 6,000, ukubwa sawa na wa eneo la Wales nchini Uingereza.

Kipande hicho cha barafu kina ukubwa mara 50 kushinda kisiwa cha Manhattan, Marekani

Satelaiti ya Marekani ilionesha jiwe hilo kubwa likiwa limemeguka ilipokuwa inapitia eneo la barafu lifahamikalo kama Larsen C Jumatano.

Wanasayansi walikuwa wanatarajia hilo. Wamekuwa wakifuatilia ufa mkubwa katika barafu ya Larsen kwa zaidi ya mwongo mmoja.

Larsen C ndiyo sehemu kubwa ya barafu iliyo kaskazini zaidi mwa dunia eneo la Antarctica.

Watafiti walikuwa awali wamesema iwapo eneo hilo lingepoteza kipande hicho cha barafu basi sehemu yote yenyewe itakuwa hatarini ya kupasuka tena siku za usoni.

Eneo la barafu la Larsen C lina kina cha mita 350.

Barafu hiyo huelea maeneo ya pembeni Antarctica Magharibi na kuzuia mito ya barafu ambayo huisaidia kukaa imara.

Watafiti wamekuwa wakifuatilia Larsen C baada ya kumeguka kwa sehemu ya barafu ya Larsen A mwaka 1995 na kisha kupasuka ghafla kwa sehemu ya barafu ya Larsen B mwaka 2002.

Wataalamu wanakadiria kwamba iwapo barafu yote kwenye sehemu hiyo ya bahari ya Larsen C itayeyuka na kuwa maji na kuingia baharini, viwango vya maji baharini vitapanda kwa sentimeta 10.

Haki miliki ya picha NASA
Image caption Ufa uliokuwa kwenye eneo hilo la barafu kabla ya kipande hicho kumeguka
Haki miliki ya picha NASA
Image caption Picha zilizopigwa Novemba mwaka jana zikionyesha ufa uliotokea
Haki miliki ya picha BAS
Image caption Kwa sasa ni katikati mwa majira ya baridi Antarctic. Ufa kwenye barafu hiyo ulipigwa picha majira ya joto yaliyopita.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii