Je unaishi katika taifa lenye watu wazembe zaidi?

Data ya mataifa yenye watu wazembe duniani
Image caption Data ya mataifa yenye watu wazembe duniani

Wanasayansi wamefanikiwa kupata data kutoka kwa watu wanaotumia simu aina ya smartphone ili kuona utendaji wao.

Chuo kikuu cha Stamford kilichanganua data ya dakika hadi dakika ya siku milioni 68 ilioonyesha kuwa kiwango cha wastani cha matembezi ya watu ni 4,961.

Hong kong ilikuwa inaongoza kwa watu wanaotembea sana ikiwa na hatua 6,880 kwa siku huku Indonesia ikiwa ya mwisho katika orodh hiyo na hatua 3,513.

Matokeo hayo hatahivyo yaligundua maelezo muhimu yanayoweza kukabiliana na tatizo la kunenepa kupita kiasi.

Simu nyingi aina ya smartphone zina programu inayoweza kurekodi hatua zinazopigwa na mtu anayetembea na watafiti walitumia data ambayo hawakuitaja kutoka kwa watu 700,000 waliotumia programu hiyo ya Argus.

Scott Delp , profesa wa uhandisi wa baiolojia pamoja na mtafiti mmoja walisema: Utafiti huo ni mkubwa mara 1000 zaidi ya tafiti nyengine zozote kuhusu matembezi ya binaadamu.

Image caption Utendaji wa baadhi ya mataifa

Kumekuwa na tafiti nzuri za afya zilizofanywa ,lakini utafiti wetu mpya kutoka kwa mataifa zaidi unafuatilia watu kila mara.

Matoko hayo yamechapishwa katika jarida asilia na waanzilishi wa utafiti huo wanasema kuwa matokeo yake yanatoa vigezo vya kuimarisha afya za watu.

Kiwango cha wastani cha hatua zilizopigwa katika taifa moja hazionyeshi umuhimu wowote wa viwango vya kunenepa kupitia kiasi kwa mfano.

Tofauti ni kati ya walio na kiwango cha utendaji wa juu dhidi ya wazembe.

Tim Wolf mmoja ya watafiti alisema: Kwa mfano , Sweden ilikuwa na pengo dogo zaidi kati ya watendaji matajiri na watendaji masikini....pia ilikuwa na viwango vya chini zaidi vya kunenepa kupitia kiasi.

Marekani na Mexico zina viwango sawa vya hatua zilizopigwa katika matembezi lakini Marekani kuna viwango vilivyo sawa vya watu wanaotembea sana pamoja na viwango vya juu vya kunenepa kupitia kiasi.

Watafiti walishangazwa kwamba tofauti ya utendaji ilitokana na tofauti kati ya wanawake na wanaume.

Katika mataifa kama vile Japan, ilio na viwngo vya chini vya ukosefu wa usawa wanaume na wanawake hufanya mazoezi kwa viwango fulani.

Lakini katika mataifa yalio na ukosefu mkubwa wa usawa, kama vile Marekani na Saudia, ni wanawake walioonekana wakitumia muda wao kutembea.

Haki miliki ya picha TIM ALTHOFF
Image caption Viwango vya matembezi ya wastani kwa dakika 30

Kundi hilo la Stamford linasema kuwa matokeo hayo yalisaidia kuelezea mfano wa meneo ambayo yana watu wengi walionenepa kupitia kiasi na kutoa mawazo mapya ya kukabiliana na tatizo hilo.

Kwa mfano waliiorodhesha miji 69 ya Marekani ambayo ina wakazi wanaoweza kutembea.

Data hiyo ya simu aina ya smartphone ilionyesha kuwa miji kama vile New York na San Fransisco walipenda kutembea hivyobasi walikuwa na viwango vya juu vya matembezi.

Huku ukihitaji gari kutembea maeneo mbalimbali kuna miji ambayo watu hawapendi kutemba kama vile Houston na Memphis.

Swala la kushangaza ni kwamba watu walitembea sana maeneo ambayo ilikuwa rahisi kutembea.