Ndege iliowabeba waandishi wa habari yaanguka Kenya

Ni ndege kama hii aina ya Cessna ilioanguka Kenya
Image caption Ni ndege kama hii aina ya Cessna ilioanguka Kenya

Ndege ndogo iliokuwa ikiwabeba waandishi habari ilianguka muda mfupi baada ya kupaa katika uwanja wa ndege wa Wilson Airport mjini Nairobi kulingana na gazeti la Daily Nation.

Ndege hiyo aina ya Cessn ilikuwa imewabeba maripoa wawili na mpiga pich mmoja kutoka kituo cha ruminga ya Citizen ambao walikuwa wanaelekea kuchukua habari za muungano wa Upinzani Nasa katika eneo la Baringo.

Waandishi hao na wafanyikazi wa ndege hiyo wamepelekwa katika hospitali ya nairobi na wanadaiwa kuwa katika hali nzuri .

Gazeti hilo linasema kuwa kamanda wa polisi wa kitengo cha anagni Rodgers Mbithi alithibitisha ajali hiyo.