Abiria asafiri kwa ndege na mkebe wa bia pekee kama mzigo

The can wrapped in a Qantas baggage tag Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mkebe huo ulifika ukiwa na kibandiko na ukiwa bado haujafunguliwa

Mwanamume mmoja amefanikiwa kusafiri na mkebe wa bia pekee kama mzingo nchini Australia.

Mwanamume huyo ambaye alitambuliwa kama Dean Stinson alisema kuwa rafiki yake alikuwa amependekeza hilo kama mzaha.

Mkebe huo ulifika ukiwa na kibandiko na ukiwa bado haujafunguliwa kama mzigo wa kwanza katika uwanja wa Perth baada ya safari ya saa nne kutoka Melbourne.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mkebe huo ulifika ukiwa na kibandiko na ukiwa bado haujafunguliwa

Shirika la ndege la Qantas lilisema kuwa haliwashauri abiria wengine kufuata mkondo huo.

Bwana Stinson aliiambia AFP kuwa alifurahi kuwa mkee huo uliwasilia salama siku ya Jumamosi.

Shirika hilo halilipishi mizigo ambayo hubebwa na abiria.