Watu wawili wakwama katika shimo kubwa Brazil

Mexico
Image caption Shimo linalotitia nchini Brazil ambamo ndani yake kuna watu wenye vyombo vya moto

Kitengo cha dharura nchini Mexico kinafanya juhudi za makusudi kutaka kuwaokoa watu wawili waliokuwa wameabiri gari ambao wamenaswa katika gari ambalo lililotumbukia katika shimo lenye urefu wa kina cha mita tano .

Shimo hilo lilionekana baada ya mvua kubwa iliyonyesha katika barabara kubwa iliyozinduliwa hivi karibuni ambayo ni kiungo baina ya mji wa Cuernavaca na Mexico City.

Gari hilo na pikipiki vilitumbukia katika shimo hilo ambalo linadhaniwa kujitengeneza kutokana na mvua kubwa Kuingilia sehemu ya barabara kuu iliyofanyiwa ukarabati kabla ya majira ya mvua.