Trump: Ninaelewana vyema na Vladimir Putin

Russian President Vladimir Putin and his US counterpart Donald Trump at the G20 summit in Hamburg, 7 July 2017 Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Putin na Trump walikutana mjini Hamburg

Rais wa Marekani Donald Trump anasema anaelewana vyema na rais wa Urusi Vladimir Putin.

Alihojiwa na kituo cha Christian Broadcasting Network, siku chache baada ya mkutano uliokuwa ukisubiriwa kati yake na Putin wakati wa mkutano wa G20 mjini Hamburg.

Trump pia amesema kuwa alikuwa na uhakika kuwa Putin angependa Hillary Clinton akiwe madarakani

Uchunguzi unaendelea kufuatia madai kuwa Urusi ilimsaidia Trump kuchaguliwa.

Trump anakana kufahamu hilo na Urusi nayo mara kwa mara imekana kuingilia kati.

"Sisi ni nguvu kubwa ya kinuklia, sawa na Urusi. haitoi maana yoyote ikiwa tutakosa kuwa na uhusiano."

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Uchunguzi unaendelea kufuatia madai kuwa Urusi ilimsaidia Trump kuchaguliwa.

Bwana Trump alitaja usitishwaji wa hivi majuzi wa mapigano kusini magharibi mwa Syria kama njia moja ya kuonyesha ushirikiano na Bwana Putin.

Trump pia alitumia mahojiano hayo kukana madai kuwa Urusi ilichangia kuchaguliwa kwake.

Mapema Trump alimtetee mwanawe Donald Trump Jr, kuhusu mkutano aliofanya na wakili wa Urusi mwaka 2016 wakati wa kampeni ya urais nchini Marekani.

Mwana wa Trump alikutana na wakili Natalia Veselnitskaya katika jumba la Trump Tower mweze Juni mwaka 2016.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mwana wa Trump alikutana na wakili Natalia Veselnitskaya katika jumba la Trump Tower mweze Juni mwaka 2016.

Mada zinazohusiana