Radi yampiga baba yake binti harusi wakati wa sherehe ya harusi

JP Nadeau beside his daughter on her wedding day Haki miliki ya picha Maggy Thomas
Image caption Radi yampiga baba yake binti harusi wakati wa sherehe ya harusi

Hakuna mtu angependa kuona harusi ikiharibika lakini baba mmoja ameshikwa na hofu kutokana na kilichotokea wakati wa harusi ya binntiye.

JP Nadeau anaripotiwa kupigwa na radi wakati akitoa hotuba huko New Brunswick, Canada.

"Wakati nilikuwa nikimuambia mkwe wangu, "Una bahati sana- Boom!!" alikimbia kituo kimoja cha habari huko Canada.

Kando na jeraha alilopata kwenye kidole chake, bwana Nadeau hakuhofu na sherehe hiyo ya harusi iliendelea.

Kila mtu alishangazwa kwanza lakini hilo halikusababisha sherehe kusitishwa.

"Ilikuwa harusi ya kufana, mke wake Nadeau aliambia kituo cha CBC.

Bwana Nadea anasema kuwa yeye ni mtu mwenye bahati kwa sababu mwaka 2015 meli alimokuwa akifanya kazi ilishika moto karibu na visisa vya Falkland, kabla ya kuokolewa na jeshi la wanahewa wa Uingereza.

Mada zinazohusiana