Gazeti la Uingereza lauita mji wa Dar es Salaam ''Kijiji cha uvuvi''

Gazeti la Uingereza lakosolewa kwa kuuita mji wa Dar es Salaam ''Kijiji cha wavuvi''
Image caption Gazeti la Uingereza lakosolewa kwa kuuita mji wa Dar es Salaam ''Kijiji cha wavuvi''

Watumiaji wa mtandao wa Twitter wanaendelea kulikosoa gazeti moja la Uingereza la Daily Mail kwa kuuita mji wa Dar es salaam ''kijiji cha wavuvi''.

Maneno hayo yalitumiwa katika habari kuhusu ziara ya klabu ya Everton nchini Tanzania.

Mtu mmoja aliitaja hatua hiyo kama utovu wa heshima na ya kibaguzi.

Haki miliki ya picha Twitter
Image caption Hivi ndivyo lilivyoandika gazeti hilo la Uingereza

Maneno hayo hatahivyo yameondolewa katika habari hiyo ambayo bado iko katika mtandao lakini bado yametumika katika maelezo ya picha, imesema.

''Mashabiki wa Bollasie wamejaa katika kijiji cha uvuvi mashariki mwa pwani ya taifa hilo'', yalisema maelezo hayo ya picha

Mada zinazohusiana