Rooney amtaka makamu wa rais wa Tanzania kuunga mkono Everton

Wachezahi wa Everton wakiongozwa na Wayne Rooney Kushoto Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wachezahi wa Everton wakiongozwa na Wayne Rooney Kushoto

Furaha imetawala miongoni mwa mashabiki wa soka nchini Tanzania kabla ya mechi ya kirafiki kati ya klabu ya Everton na Gor Mahia ya Kenya katika uwanja wa kitaifa wa Dar es Salaam ulio na uwezo wa kubeba mashabiki 60,000.

Wachezaji wa Everton walipata makaribisho ya kifalme tangu kuwasili kwao siku ya Jumatatu katika taifa hilo la Afrika mashariki.

Mchezaji wa timu ya taifa ya Uingereza Wayne Rooney amevutia umati mkubwa wa mashabiki na wengi wanamsubiri kumuona akicheza katika mechi hiyo.

Mchezaji wa DR Congo Yannick Bolasie alishindana na Rooney kwa kuvutia wafuasi huku mashabiki wa DR Congo wakimtembelea Bollasie.

Walivalia tisheti zenye uso wake.Hatahivyo ni Rooney aliyekuwa kivutio kikuu miongoni mwa mashabiki.

Pia makamu wa rais Samia Suluhu Hassan alikubaliana na hilo.

''Wayne Rooney alinifanya kuiunga mkono Manchester United na sasa sijui nifanyeje kwa sababu amehamia Everton'', alisema.

Na Rooney alimjibu.

''Uwepo wangu hapa ni ni uzoefu wangu mpya na natumai kwamba makamu wa rais sasa ataweza kuiunga mkono Everton''.

Mada zinazohusiana