Trump na Merkel waongoza kumbukumbu za mshindi wa tuzo ya Nobel Liu Xiaobo

Liu Xiaobo alikua mtu maarufu zaidi nchini China
Image caption Liu Xiaobo alikua mtu maarufu zaidi nchini China

Rais Trump na kansela wa Ujerumani Angela Merkel wameongoza kumbukumbu za mchina aliyeshinda tuzo ya amani ya Nobel Liu Xiaobo, ayelikufa kutokana na saratani ya ini.

Image caption Trump ameelezea kusikitishwa na kifo hicho

Hata hivyo, serikali ya Beijing ambayo ilimhukumu kifungo cha miaka kumi jela kwa tuhuma za kutaka kupindua serikali haijatambua kifo chake.

Image caption Kukosekana kwa Liu katika tuzo za mwaka 2010 kuliwakilishwa na kiti pekee

Mpaka sasa taarifa ya kifo chake haijatajwa katika vyombo vya habari vya nchi hiyo, huku taarifa kutoka vyombo vya kimataifa zikichujwa nchini China.

Mshindi wa tuzo ya Nobel China, Liu Xiaobo, aaga dunia

Merkel amesifu ujasiri wa Liu Xiaobo huku Trump nae akisema amesikitishwa na taarifa za kifo cha mtu ambae alijitolea maisha yake kwa ajili ya demokrasia.