Trump na Macron kuadhimisha siku maalum ya Ufaransa

Emmanuel Macron (kushoto) na Trump wakiwa katika picha ya pamoja katika ikulu ya Paris
Image caption Emmanuel Macron (kushoto) na Trump wakiwa katika picha ya pamoja katika ikulu ya Paris

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron atamualika Donald Trump katika maadhimisho ukombozi wa Ufaransa mjini Paris leo hii.

Viongozi hao watatizamavikosi vya jeshi la Ufaransa na Marekani vikiungana pamoja miaka mia moja baada ya vita ya kwanza ya dunia.

Walizungumza siku ya Ijumaa na Trump kusema kuwa Marekani inawez kubadili msimamo wake juu ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Macron baadae atasafiri mpaka mji wa Nice kujumuika na wakazi wake katika kumbukizi ya mwaka mmoja tokea shambulizi la kigaidi lililosababisha vifo vya watu 14 kufanyika.