Jaji adhoofisha marufuku ya Trump dhidi ya mataifa 6 ya Kiislamu

Bibi na babu pamoja na jamaa wengine wa watu wa familia zinazoishi Marekani hawawezi kuzuiwa kuingia nchini humo chini ya marufuku ya rais Trump Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Bibi na babu pamoja na jamaa wengine wa watu wa familia zinazoishi Marekani hawawezi kuzuiwa kuingia nchini humo chini ya marufuku ya rais Trump

Bibi na babu pamoja na jamaa wengine wa watu wa familia zinazoishi Marekani hawawezi kuzuiwa kuingia nchini humo chini ya marufuku ya rais Trump , jaji mmoja ameamuru.

Agizo hilo la jaji wa wilaya Judge Derrick Watson katika jimbo la Hawaii, ni pigo jipya kwa marufuku hiyo.

Jaji huyo alisema kuwa marufuku hiyo haikuelewa vizuri agizo la mahakama ya juu .

Uamuzi huo uliotolewa mwezi uliopita, uliidhinisha kwa uchache marufuku hiyo dhidi ya wakimbizi na wanaozuru taifa hil kutoka kwa mataifa sita ya kiislamu.

Ulisema kuwa wale walio na familia zao wataruhusiwa kuingia Marekani.

Lakini utawala wa Trump uliamua kwamba uamuzi huo haukuhusisha bibi na babu pamoja na wajukuu, mashemeji ,wajomba, mashangazi, mpwa wa kiume na wa kike na binamu.

Jaji huyo alishutumu uelewa wa serikali kuhusu watu wa karibu wa familia.

Ukweli ni kwamba, kwa mfano watu wa karibu wa familia wanashirikisha bibi na babu.

Bibi na Babu ndio chanzo cha watu wa karibu wa familia,aliandika.

Mahakama ya juu bado inaangazia jaribio la kuwazuia raia wa Iran,Libya, Somalia, Sudan, Syria na Yemen kuingia nchini Marekani.

Mahakama iliamuru marufuku ya muda kutekelezwa mnamo mwezi Mei.

Bwana Trump anasema kuwa vikwazo hivyo vinahitajika ili kuimarisha usalama wa Marekani dhidi ya mashambulio ya kigaidi.

Hatahivyo wakosoaji ikiwemo majimbo na makundi yanayopigania makundi ya wakimbizi yamesema kuwa marufuku hiyo inawabagua Waislamu.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii