Diabate: 'Niliambiwa wanawake kama mimi hawafai kucheza ala za muziki'

Diabate: 'Niliambiwa wanawake kama mimi hawafai kucheza ala za muziki'

Mwanamuziki Salimata Diabate kutoka Burkina Faso analenga kuwahamasisha wanawake zaidi kuanza kucheza ala za muziki za kitamaduni.

Kabla ya kufika alipo, alikumbana na changamoto nyingi zikiwemo kuambiwa kwamba wanawake hawafai kucheza ala za muziki.

Bi Diabate kwa sasa ni mwanamuziki mashuhuri na mcheza ala kwa jina balafon na anatumai wanawake wengine watamuiga.