Trump ajiunga na Macron kwenye gwaride Sikukuu ya Bastille jijini Paris

President Trump and First Lady Melania on Bastille Day Haki miliki ya picha AFP
Image caption Trump amewasifu sana wenyeji wake Macron na mkewe Brigitte

Rais wa Marekani Donald Trump ameungana na mwenzake wa Ufaransa Emmanuel Macron kwenye gwaride jijini Paris kama sehemu ya maadhimisho ya Sikukuu ya Bastille ambayo huadhimishwa kila mwaka tarehe 14 Julai.

Wanajeshi wa Marekani na Ufaransa wameandaa gwaride kwa pamoja Champs-Élysées.

Gwaride hilo, ambalo limetumiwa kuadhimisha miaka 100 tangu Marekani ilipoingia katika Vita vya Kwanza Vikuu vya Dunia, pia imehusisha farasi, ndege za kivita na helikopta.

Rais Macron, akiwa kwenye gari la kijeshi, amekagua gwaride hilo.

Awali, Bw Trump alisema "vita vya kupigania uhuru" viliunganisha Marekani na Ufaransa.

Bw Macron baadaye amezuru mji wa Nice kujiunga na maadhimisho ya mwaka mmoja tangu shambulio la kigaidi ambapo mwanamume mzaliwa wa Tunsiia alivurumisha lori kwenye watu waliokuwa wakisherehekea ufukweni na kuua watu 86.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Macron akikagua gwaride lililoandaliwa na wanajeshi
Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wanajeshi wa Marekani mwaka huu wamejiunga kwenye gwaride

Mnamo Alhamisi, Bw Trump alidokeza kwamba huenda akabadili msimamo wake kuhusu mabadiliko ya tabia nchi, baada ya Bw Macron kuutetea mwafaka wa Paris wa mwaka 2015.

"Jambo huenda likatokea kuhusu mwafaka wa Paris," Trump alisema. "Hebu tusubiri."

Alhamisi, mke wa rais wa Marekani Melania Trump ametembelea kanisa kuu la Notre Dame akiwa na mwenzake wa Ufaransa Brigitte Macron.

Ufaransa imesalia kuwa kwenye hali ya tahadhari kutokana na mashambulio ya kigaidi.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii