Kwa Picha: Picha bora Afrika 7 -13 Julai 2017

Mkusanyiko wa picha bora Afrika na kuhusu Waafrika wiki hii.

Robert Kyagulani, 11 July 2017. Haki miliki ya picha AFP
Image caption Jumanne, nyota wa muziki wa reggae nchini Uganada Robert Kyagulani, maarufu kama Bobi Wine, alionekana mwenye furaha baada ya kuapishwa kuwa mbunge katika ucahguzi mdogo uliofanyika mwezi uliopita. Aliwania kama mgombea huru. Ameahidi kutetea maslahi ya watu maskini bungeni. to champion the interests of the poor in parliament.
Kinshasa Haki miliki ya picha AFP
Image caption Picha hii iliyotolewa Jumatatu inawaonesha waumini wa kundi linalojiita Wajumbe wa Wahenga wakitekeleza tambiko la kidini katika mji mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Kinshasa...
Koko Lunda Kamosi Haki miliki ya picha AFP
Image caption ... na hapa kiongozi wao Koko Lunda Kamosi anaonesha maandishi ya Nati-Kongo na alfabeti yake ya abjadi 23. Kundi hilo hutetea kurejeshwa kwa dini za Kiafrika ambazo zilitoweka au kufifishwa kutokana na ukoloni na kuingizwa kwa Ukristo barani Afrika.
Sheikh Ahmed Mohammed Awal Monrovia, Liberia on 9 July 2017 Haki miliki ya picha EPA
Image caption Jumapili, raia hawa wa Liberia wanaonekana wakimpiga picha msomi wa Kiislamu kutoka Marekania ambaye alikuwa anawahutubia katika uwanja wa michezo mjini Monrovia...
Sheikh Ahmed Mohammed Awal Monrovia Haki miliki ya picha EPA
Image caption Sheikh Ahmed Mohammed Awal alizuru Liberia, taifa lililoanzishwa na watumwa wa zamani, kama sehemu ya juhudi zake za kueneza dini ya Kiislamu.
Han Hyun-Min Seoul. Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mwanamitindo anayechipuka nchini Korea Kusini Han Hyun-Min, ambaye babake ni raia wa Nigeria, hapa anapambwa kabla ya kupigwa picha mjini Seoul. Anaendelea kuvuma licha ya ubaguzi dhidi ya watu weusi, ambao wakati mwingine huitwa hata 'mbwa'.
Bingerville, near Abidjan. Haki miliki ya picha AFP
Image caption Na Jumatatu, mfanyakazi wa kampuni ya kusambaza umeme Ivory Coast anafanyia majaribio ndege isiyokuwa na rubani ambayo itatumiwa na taifa hilo kuchunga na kulinda nyaya za umeme na mfumo wote wa kusambaza umeme.
Tunis Haki miliki ya picha AFP
Image caption Tunisia, vijana nao wanashiriki mchezo wa Super Nintendo wakati wa hafla ya kufungwa kwa makala ya pili ya maonesho ya Comic Con Tunisia Jumapili katika mji wa Le Kram town, kaskazini mwa jiji kuu la Tunis.
Raila Odinga, Nairobi, Kenya, 7 July 2017 Haki miliki ya picha EPA
Image caption Uchaguzi unakaribia nchini Kenya, na mnamo Ijumaa wanaume hawa walihudhuria mkutano wa kampeni Ijumaa jijini Nairobi wakiwa wamevalia mavazi ya kuchekesha, na kufikisha ujumbe kupigia debe mgombea wa chama cha upinzani cha Orange Democratic Movement (ODM)...
Kenya, 7 July 2017. Haki miliki ya picha EPA
Image caption Siku hiyo pia, wachezaji wa kutumia vikaragosi wakiwa na ujumbe mzito wakati wa mkutano wa kuhimiza amani uchaguzini ambao ulihudhuriwa na Rais Uhuru Kenyatta, ambaye anawania kuongoza kwa muhula wa pili.
Cairo, Egypt, 12 July 2017. Haki miliki ya picha EPA
Image caption Nchini Misri, siasa zilikuwa mbali sana na fikira za watoto hao. Waliwapeleka farasi wao wakaogelee kiasi katika ziwa moja Cairo angalau kukwepa jua kali.
IAAF
Image caption Nchini Kenya, kuanzia Jumatano taifa hilo limekuwa likiandaa makala ya kumi na ya mwisho ya mashindano ya ubingwa wa riadha duniani kwa wanariadha wasiozidi umri wa miaka 18. Mashabiki hao walionesha upendo wao kwa taifa la Kenya.
IAAF
Image caption Mwanariadha huyu wa Ethiopia naye alionekana kuwa tayari kabisa 'kuufukuza upepo'!

Picha kwa hisani ya AFP, EPA, Getty Images, Reuters na Peter Njoroge, BBC.

Mada zinazohusiana

Kuhusu BBC